

Lugha Nyingine
三明表彰海西三明生态工贸区开发建设先进单位
![]() |
Picha iliyopigwa tarehe 24 Julai 2025 ikionyesha hafla ya uzinduzi wa aina mpya za magari ya chapa ya SOUEAST mjini El Alamein, Misri. (Xinhua/Sui Xiankai) |
CAIRO - SOUEAST, chapa ya magari ya China, imezindua aina nne mpya za magari nchini Misri jana Alhamisi, ikionyesha upanuzi mkubwa wa chapa hiyo katika soko la Afrika.
Uzinduzi huo uliofanyika katika mji wa Alamein, kaskazini mwa Misri huku aina nne mpya za magari karibu sehemu zote za soko la SUV, ambazo ni SUV S09 kinara ya kistarehe ya kisasa, SUV S07 C-segment ya kisasa ya kimjini, SUV S06 ya mtindo wa mjini, na SUV S05 ya usanifu wa mjini.
Yuan Anguo, mkuu msaidizi wa SOUEAST tawi la Kimataifa, amesema kuwa magari hayo yameundwa kukidhi mahitaji mbalimbali ya madereva, yakitoa mchanganyiko wa mtindo, ufanisi, na teknolojia ya hali ya juu.
"Maono ya SOUEAST ni kuwezesha vijana zaidi duniani kote kuwa na mazingira rahisi ya usafiri mijini," amesema Yuan kwenye hafla hiyo ya uzinduzi, akisisitiza imani kubwa ya SOUEAST katika soko la Misri.
Hadi kufikia mwisho wa 2025, SOUEAST inalenga kuanzisha maduka 15 na vituo vitano vya huduma baada ya mauzo nchini Misri, Yuan ameeleza, akisema kuwa aina mbili mpya kabisa za magari za knocked down (CKD) zitaingizwa sokoni kati ya 2026 na 2027.
Kwa uwepo katika nchi na maeneo zaidi ya 30, chapa hiyo ya magari imeanzisha zaidi ya mitandao 140 ya mauzo na huduma duniani kote.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma